The world is changed by examples, not by opinions

The world is changed by examples, not by opinions

Tuesday, 31 December 2013

HUZUNI SANA
KIJANA APANDA JUU YA MNARA WA SIMU LEO UBUNGO JIJINI DAR NA KUGOMA KUSHUKA MPAKA AONANE NA RAIS KIKWETE
Askari wa kikosi cha zima moto ilibidi wafanye kazi ya ziada kumwokoa kijana huyu aliyepanda juu ya mnara wa simu ubungo jijini Dar akitaka kuonana na rais amweleze yale yaliyomsibu ikiwemo kubambikiwa kesi na jeshi la polisi na kuhukumiwa jela miezi sita
hapo askari wakipanda tayari kwa kumwokoa
hapa akiwa kabebwa begani tayari kurudi chini

daah! Alhamdullillah Mungu kaepushia mbali
Kwa kweli hatujui ukweli wa mambo kuhusu madai yake ila rais na selikali yake haiwezi kubisha jinsi polisi na mahakama zilivyofinya haki za watanzania
wapo wanaouawa bila hatia na hilo jeshi na mifano hai ipo, wapo wanaobakwa mifano hai ipo, wapo kama hivyo wanaokwenda jela bila hatia , ukienda katika jela zetu utakuta watoto wenye umri wa miaka chini ya 18 wamefungwa pamoja na watu wazima na kesi zimerundikana mahakamani, ni huzuni tena huzuni sana watu wanakaa kizuizini bila ya kusikilizwa kesi zao tena kwa miaka na miaka  kwa sababu tu ya rushwa inayoendelea katika mahakama zetu .....eee mungu tusaidie! 

No comments:

Post a Comment